Msemo huo wa waChina ungeweza kuwa hata msemo wa waTanzania.

Matatizo ya kila siku ni mengi, kiasi kwamba ingeweza kumfanyia mtu akate tamaa. Lakini kwa hatua moja kwa siku ya leo nguvu bado atakuwa nayo ya kutosha. Tena kama hajisikii peke yake njiani.

"Hatua" maana yake ni "twende mbele".

Tunasindikiza watu wa Tanzania kwenye njia yao wanaotaka kupiga hatua walau moja.

Tunawapa moyo kwa kusaidia na kiasi kidogo na mara moja tu ili waendelee kujitegemea.

Hatuna gharama la uendeshaji, bali tunasaidia watu wa kawaida wanaojitahidi wenyewe katika maendeleo.

Tunasisitiza kwamba fedha iende moja kwa moja kwa watu bila kupunguzwa.